Ghana yasitisha uuzaji wa nafaka nje kutokana na ukame wa mazao

Baada ya Nigeria au Côte d’Ivoire, ni zamu ya Ghana kusitisha mauzo yake ya nafaka. Uamuzi unaanza kutumika mara moja na hadi hatua nyingine itakapochukuliwa. Uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatatu Agosti 26, 2024 na Waziri wa Kilimo. Sababu: ukame mkali ambao unaathiri sana uzalishaji na, kulingana na mamlaka, unatishia nchi na uhaba wa chakula.

Maeneo sita ya kaskazini na mashariki mwa Ghana pekee yanatoa takriban 62% ya nafaka nchini humo. Na yote yanaathiriwa na ukame. Hali ambayo imekuwa ikiendelea kwa miezi miwili, na ambayo tayari imesababisha hasara kwa wakulima karibu nusu milioni, kulingana na serikali.

Matokeo yake, mamlaka inasema kunaripotiwa uhaba wa mchele, mahindi na soya... bidhaaza msingi za mlo nchini Ghana. Kwa kujibu, Bryan Acheampong, Waziri wa Kilimo, alitangaza siku ya Jumatatu kusitishwa kwa mauzo ya bidhaa hizi. Hatua ambayo serikali inakusudia kuandamana nayo na ufadhili: kunahitajika dola milioni 500, sehemu yake kutoka Benki ya Dunia.

Hatari ya mfumuko wa bei

Wakati huo huo, Waziri wa Fedha, Mohammed Amin Adam, alionyesha kuwa Ghana itatumia hifadhi ya nafaka ya ECOWAS na "kushirikiana na sekta ya kibinafsi" kuagiza nafaka zilizokosekana.

Uamuzi usio na hatari: kulingana na waziri mwenyewe, uagizaji kama huo unaweza kudhoofisha sarafu na kuongeza mfumuko wa bei ya chakula: hali hii ilizidi 24% mnamo mwezi Juni 2024.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii