Watoto milioni 10 hawasomi baada ya mafuriko makubwa barani Afrika

Kwa mujibu wa shirika la Save the Children, watoto milioni 10 kwa sasa hawasomi nchini Nigeria, Mali, Niger na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Shule zimeharibiwa au kutotumika kwa sababu ya maji kuongezeka, familia zimehama makazi, mwaka wa shule kuahirishwa... shirika hili linatoa wito kwa serikali na washirika kuchukua hatua za dharura.

Mafuriko yanazidisha mzozo wa elimu, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children. Wanafunzi milioni 10 ambao kwa sasa wamekwama nyumbani au waliokimbia makazi yao kwenye idadi ya watoto milioni 36, ikiwa ni pamoja na milioni 20 nchini Nigeria pekee, ambao tayari hawasomi katika nchi hizi nne, kulingana na Umoja wa Mataifa, kutokana na migogoro na umaskini.

Mwishoni mwa mwezi wa Septemba, Niger ilitangaza kuahirishwa kwa mwaka wa shule kwa angalau wiki tatu kutokana na mafuriko. Katika nchi hii ambapo shule tayari zimejaa kupita kiasi wanafunzi, zaidi ya madarasa 5,000 yameharibiwa au kujaa maji. Mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba, Mali pia iliainisha kwamba inahirisha mwaka wa shule. Nchini Nigeria, majimbo thelathini kati ya thelathini na sita yameathiriwa na mafuriko. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mkoa wa Tanganyika ndio ulioathiriwa zaidi.

Save the Children inatoa wito kwa wafadhili kuunga mkono mwitikio ulioimarishwa kwa matokeo ya majanga ya asili. Kwa mujibu wa shirika huili lisilo la kiserikali, serikali na washirika lazima wachukue hatua haraka ili kutoa ofa mbadala zinazoruhusu watoto kuendelea na masomo. Kulingana na Save the Children, pia tunahitaji shule nyingi zaidi zinazostahimili hali ya hewa, ambazo zimekuwa za mara kwa mara na ambazo mwitikio wa kimataifa lazima ujumuishe mahitaji na haki za watoto.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii