Mwanaume amfukuza mke kisa tatoo

Mchungaji aliyejulikana kwa jina la Geor Davie ameshangaa baada ya kufahamu kwamba mmoja wa wafuasi wake alifukuzwa na mumewe baada ya kuamua kachorwa tattoo ya jina lake (mchungaji). 

 pasta huyo, mtumishi wa Mungu alishangaa mwanamke huyo mwenye tattoo yake ni nani na kumtaka ajitokeze. 

"Mama nini kilikufanya unipende kiasi hicho?" aliuliza mchungaji kutoka kwenye mimbari. 

"Mchungaji nakupenda lakini ninapitia mengi; mume wangu aliniacha kwa sababu ya hii tattoo. Aliniuliza kwa nini nilikuchora na yeye bado yupo?" Alisema mwanamke huyo.

 Mchungaji akiwa amepigwa na butwaa alijiuliza ni kwa namna gani mwanaume anaweza kumwacha mwanamke mrembo namna ile. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii