Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga leo Oktoba 6, 2024 ameanza ziara yake ya siku 4 Katika wilaya ya Kiteto Mkoani humo na kukagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji Nchinila.
Akiwa katika Kata ya Dosi Dosi, Sendiga amekagua ujenzi wa Nyumba ya mganga wa Zahanati ya Nchinila na kumuagiza Mkurugenzi Halmashauri ya Wiliya ya Kiteto, CPA Hawa Hassan kutenga Shilingi milioni 20 kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba hiyo.