Kisa Shilingi 200: Rasta auwa Mtu Morogoro

Mkazi wa Kijiji cha Sinyaulime Tarafa ya Ngerengere Wilaya na Mkoa wa Morogoro, Kulwa Bosco (27),  anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Hussein Steven (35), mkazi wa Ngerengere Kaskazini.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Septemba 29, 2024, katika kitongoji cha Ngerengere Kaskazini Kata ya Ngerengere Wilaya ya Morogoro vijijini.

Amesema, chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliosababishwa na kubishania shilingi mia mbili wakiwa katika mchezo wa kamari ya Pool table kwenye baa ya Itonyange maarufu kama Maokoto, na ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma Hussein.
Kufuatia tukio hilo, Polisi Mkoa wa Morogoro imewataka Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wajikite kwenye kufanya kazi, ili kuingiza kipato cha halali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii