MIILI YA WATU WATATU YAKUTWA MSITUNI IKIWA IMECHOMWA MOTO KWENYE IST

Jeshi la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kuwatambua watu watatu ambao miili yao ilikutwa imechomwa moto ndani ya gari dogo aina ya IST katika Msitu wa Hifadhi, kijiji cha Sinden, wilayani Handeni.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, akieleza kuwa tukio hilo la kusikitisha limemhusisha Mkaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Jonasia Edward Shayo, pamoja na familia yake ya watu wawili.


Kamanda Mchunguzi amesema kwamba miili ya marehemu hao ni ya Jonasia Edward Shayo, mwanafunzi wa darasa la tatu ambaye ni mtoto wake, pamoja na mke wake.


Inadaiwa kuwa watu hao walifungiwa ndani ya gari aina ya IST na kisha gari hilo kuchomwa moto, katika kitendo kinachochunguzwa kwa sasa kama mauaji ya kutisha. Aidha, jeshi la polisi limeanzisha uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha tukio hilo na wahusika waliotekeleza uhalifu huo.


Kamanda Mchunguzi ameahidi kwamba vyombo vya dola vitafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha haki inatendeka na wahalifu wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii