Familia moja katika Kijiji cha Akipeneti, Kata Ndogo ya Buteba, Wilaya ya Busia, imefanya mazishi ya ishara kwa mgomba.
Hatua hii ilichukuliwa baada ya kutomwona mwanao,Kennedy Were Wanga, kwa miaka miwili bila mafanikio.
Kennedy Were Wanga alitekwa nyara mnamo Aprili 23, 2022, huko Nambaale, Busia-Kenya, na watu waliokuwa na bunduki waliokuwa wakitumia gari ambayo haina usajili ,Tangu wakati huo, hajaonekana wala kusikika, akiwa hai au amekufa.
Kabla ya kupotea, Wanga, ambaye alikuwa Katibu wa Ulinzi wa Kijiji cha Akipeneti, alikuwa anajihusisha na biashara ya uchimbaji wa dhahabu.
Kulingana na familia yake iliamua kuzika mgomba badala ya mwili wake kuto kuonekana na wazee wa kijiji na viongozi wa kanisa walishauri wazike mgomba.
Dada yake mdogo, Maureen Wanga, alisema mazishi hayo ya kiishara yalikuwa hatua muhimu ili kusaidia roho ya ndugu yake kupata amani.
"Tulinunua suti nzuri, tukavisha mgomba, na kuliweka ndani ya jeneza. Tunaamini hili litaruhusu roho yake ipumzike kwa amani," alisema Maureen.
Alieleza kuwa familia hiyo ilitafuta magerezani na vituo vya polisi kote Kenya kwa miaka miwili na nusu lakini hawakupata chochote.