Tshisekedi ataka Rwanda iwekewe vikwazo kwa kuunga mkono M23

Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo ametoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuchukuwa vikwazo dhidi ya Rwanda kutokana na kile alichokiita kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la serikali mashariki mwa DRC.

Rais Tshisekedi amesema hayo wakati Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini NewYork ikiwa ni siku ya tatu tangu mkutano huo uanze. 

Tshisekedi amesema uchokozi wa Rwanda unakiuka uhuru wa DRC huku akisisitiza kuwa kuibuka tena kwa kundi la M23 kumesababisha mgogoro wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa na kwamba  Rwanda  inawajibika katika kuvuruga utulivu wa nchi hiyo.

Kwa miongo kadhaa sasa, eneo la mashariki mwa Kongo lenye utajiri mkubwa wa madini limekuwa likishuhudia ghasia za makundi yenye silaha ambazo zimesababisha maafa makubwa.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuhutubia juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja nachangamoto zinazoikabili dunia hususan vita na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii