BUSTANI ya Uhuru Park imefungwa tena kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z.
Japo serikali ya Kaunti ya Nairobi na ile ya kitaifa hazijatoa kiasi kamili cha hasara iliyokadiriwa wakati wa maandamano ya vijana hao, Uhuru Park na Central Park zitafungwa ili kutoa nafasi kwa serikali kufanya ukarabati.
Maandamano hayo ya kukosoa serikali ya Rais William Ruto, yalianza miezi miwili iliyopita.
Bw Ibrahim Otieno, ambaye ni Afisa wa kaunti anayesimamia masuala ya Mazingira, alisema kuwa bustani ya Uhuru itafunguliwa baada ya serikali kufanya ukarabati.
Lango la kuingia kwenye bustani hiyo liliharibiwa.
Kando na hayo, ndege ya zamani ya Boeing 737 ambayo ilikusudiwa kutumika kama mkahawa na kituo cha burudani iliteketezwa na hata vifaa vingi, vikiwemo vyoo viliharibiwa.
“Waliharibu vyoo vyote na kuteketeza basi. Uharibifu ulikuwa mkubwa sana,” Bw Otieno aliambia