Madai ya Israeli kumuua Deif yamekuja ikiwa imepita siku moja baada ya kuuawa kwa mkuu wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran, maujai ambayo yalithibitishwa na Iran na Hamas.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Israeli, IDF, Mohammed Deif aliuuawa katika shambulio la ndege za kivita katika eneo la Khan Yunis tarehe 13 ya mwezi Julai.
Israeli inasema Deif alipanga na kutekeleza shambulio la tarehe saba ya mwezi Oktoba katika ardhi yake, shambulio ambalo watu 1,197 waliuuawa kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Israeli.
Idara ya afya katika ukanda wa Gaza inayoongozwa na wapiganaji wa Hamas ilisema kwamba watu zaidi ya 90 walikuwa katika eneo kulikotokea shambulio la tarehe 13 mwezi Julai lakini ilikana kuwepo kwa Deif.
Jeshi la Israeli pia limedai kuwa Deif katika kipindi cha miaka mingi amekuwa akitekeleza mashambulio dhidi ya ardhi yake.