Rais wa Iran kuapishwa: Baada ya miezi miwili madarakani, Massoud Pezeshkian ashindwa kujizatiti

Rais mpya wa Iran Massoud Pezeshkian ataapishwa mbele ya Bunge leo Jumanne Julai 30. Kisha atakuwa na siku 15 za kuwasilisha mawaziri wake kwenye Bunge kwa ajili ya kupigiwa kura ya imani mbele ya baraza linaloundwa na wahafidhina. Lakini kama atawasilishwa kama mwanamageuzi, wengi wanatilia shaka lebo hii.

Tangu aingie madarakani, ukandamizaji haujapungua. "Tangu kifo cha rais, tulikuwa na "ombwe la kisiasa", hivyo tungeweza kutarajia nchi hii itapooza kidogo. Siku hiyo hiyo, kiongozi mkuu alikuja kutoa hotuba akisema, "msijali, hakuna kitakachobadilika", hali ambayo tayari ilimaanisha kwamba mamlaka inabaki mikononi mwake," Kian Habibian, Muirani aliye uhamishoni nchini Ufaransa, anaelezea RFI na mwanzilishi mwenza wa shirika la Wanafunzi wa Iran la We are Iranian Students. “Iwapo kuna rais au la, kamata kamata itaendelea, kwa sababu maagizo yanatoka juu, kutoka kwa kiongozi mkuu, mamlaka ya kidini na walinzi wa mapinduzi. Kukiwa na rais au la, ukandamizaji na mauaji yanaendelea nchini Iran. "


Hali ngumu kwa Massoud Pezeshkian

Lakini mashaka pia yanaendelea, kwa sababu zaidi ya wiki tatu baada ya kuchaguliwa kwake, rais mpya wa Iran, mwanamageuzi Massoud Pezeshkian, bado hajaweka muhtasari mpana wa sera yake. Kwa Reza, mfanyabiashara wa miaka ya sitini, rais mpya lazima kwanza ashughulikie masuala ya kiuchumi, hasa kuondolewa kwa vikwazo, lakini pia kulegeza vikwazo vya mavazi kwa wanawake au kupunguza vikwazo kwenye mtandao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii