Bustani ya Mnazi mmoja kuwa chachu ya Utalii

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi kutunza mazingira na kuweka haiba ya mji kuwa safi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo leo Julai 15, 2024 wakati alikizindua Bustani ya Mnazi Mmoja, iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Amesema, lengo la bustani hiyo ni kwa ajili ya mapumziko kwa wageni wanaotembelea vivutio vya utalii na Wananchi wanao kwenda kuwaangalia wagonjwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja.

Dkt. Mwinyi pia ameipongeza Kampuni ya Infinity Development na Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa kujenga bustani hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii