Kundi la wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza la Hamas, limesema mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano yanaendelea na Kamanda wake wa kijeshi Mohammed Deif yuko katika hali nzuri kiafya.
Taarifa hiyo ya Hamas ilitolewa jana, siku moja baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi yaliyomlenga kamanda huyo wa Hamas ambayo imeleezwa na maafisa wa afya kwamba yaliwauwa takriban watu 90 wakiwemo watoto.
Mnamo siku ya Jumamosi waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema bado hawana uhakika ikiwa Deif ameuwawa. Mohammed Deif anatajwa kuwa ndiye kinara aliyepanga shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel lililosababisha vita vya Gaza.