DCEA IMEONGOZA OPERESHENI MAALUM YA UOKOTAJI WA SINDANO ZILIZOTUMIKA JIJINI ARUSHA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) tarehe 22.08.2024 imeongoza kampeni maalum ya uokotaji wa sindano kwenye mazingira hatarishi ambazo zimeshatumika na waraibu wa dawa za kulevya jijini Arusha.
Zoezi  hilo maalum  lilifanyika katika maeneo ya Darajani, Ngarenaro na Ungalimited yaliyopo  Arusha mjini lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inabaki salama dhidi ya madhara yatokanayo na utupaji hovyo wa sindano ambazo zimeshatumika.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano pamoja na kuziwezesha Asasi hizo ili ziweze kufanya shughuli zake za kila siku kwa ufanisi na weledi kwenye jamii hasa zile hatarishi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii