Almasi ya pili kwa ukubwa duniani yagunduliwa nchini Botswana

Almasi kubwa ya kipekee, ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani kwa karati 2,492, na ambayo haitoshi kwa urahisi kwenye kiganja cha mkono, imepatikana kwenye mgodi mmoja nchini Botswana, kampuni ya uchimbaji madini ya Canada imetangaza siku ya Alhamisi.

Jiwe hili la thamani, lililogunduliwa katika mgodi wa Karowe kaskazini mashariki mwa Botswana, mzalishaji mkuu wa almasi barani Afrika, ni "moja ya almasi kubwa zaidi kuwahi kugunduliwa", inabainisha kampuni ya Lucara katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kulingana na serikali ya Botswana na wataalamu kadhaa, itakuwa ya pili kwa ukubwa kuwahi kupatikana duniani. Kwa upande wa karati, sio mbali na almasi kubwa zaidi inayojulikana ulimwenguni, "Cullinan", ya zaidi ya karati 3,100, iliyogunduliwa nchini Afrika Kusini mnamo mwaka 1905.

taarifa kwa vyombo vya habari, ambaye hakutoa maelezo yoyote juu ya thamani ya ugunduzi au ubora wake.

Almasi hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa Rais Mokgweetsi Masisi, ambaye anasema ni kubwa zaidi kuwahi kupatikana katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, na pia kwa waandishi wa habari mjini Gaborone.

"Ugunduzi wa kihistoria wa almasi hii, muhimu zaidi katika miaka 120, unafurahisha," anasisitiza Tobias Kormind, mkurugenzi mkuu wa 77 Diamonds, sonara mkubwa zaidi wa mtandaoni barani Ulaya.

Botswana ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa almasi duniani, ambayo ni chanzo chake kikuu cha mapato, ikiwakilisha 30% ya Pato la Taifa na 80% ya mauzo yake nje.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii