Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati sakata la binti anayedaiwa kudhalilishwa kwa kubakwa na kulawitiwa na watu watano waliodaiwa kutumwa na afande kufanya jambo hilo likiendelea kufanyiwa uchunguzi.
Waziri Gwajima amesema kuwa lazima haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na siyo vinginevyo.
Anaoa kauli hiyo baada ya kusambaa habari katika mitandao ya kijamii iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya kuwa jalada la kesi ya vijana hao limekamilika lakini uchunguzi wa jeshi hilo umebaini binti huo alikuwa kama anajiuza ‘kahaba’ na kwamba vijana jao watano hawakutumwa na askari kama ilivyoelezwa awali.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri Gwajima kupitia mitandao ya kijamii amesema amepokea ‘tags’ nyingi za maoni na maswali kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC Mkoa wa Dodoma juu ya mwenendo wa shauri la binti hiyo anayedaiwa kukaa Yombo jijini Dar es Salaam.
“Ndugu wananchi, nimepokea hisia zenu, maoni na maswali yenu ambayo mmeelekeza kwangu, nimewasiliana na Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye