UN yalaani idadi visa vya unyanyasaji dhidi ya wahudumu wa masuala ya kibinadamu

Umoja wa Mataifa unashutumu ghasia "zisizokubalika" ambazo zimekuwa zikifanyika dhidi ya wahudumu wa masuala ya kibinadamu, ambapo 280 kati yao wameuawa duniani kote mwaka 2023, rekodi iliyochochochewa na vita huko Gaza na ambayo iko katika hatari ya kupada mwaka 2024.

"Kuhalalisha unyanyasaji dhidi ya wahudumi wa masuala ya kibinadamu na ukosefu wa uwajibikaji ni vitu ambavyo havikubaliki, haukubaliki na ni hatari sana kwa operesheni za kibinadamu kila mahali," ameshutumu Joyce Msuya, kaimu mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Jumatatu hii, Agosti 19, kwenye hafla ya Siku ya Wahudumu wa Masuala ya Kibinadamu Duniani. "Pamoja na wafanyakazi 280 wa kibinadamu
waliouawa katika nchi 33 mwaka jana, 2023 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa kwa jumuiya ya kimataifa ya wahudumu wa Masuala ya Kibinadamu Duniani", na ongezeko la 137% ikilinganishwa na mwaka 2022 (118 waliuawa), inabainisha OCHA katika taarifa kwa vyombo vya habari, kwa kutumia takwimu kutoka Hifadhidata ya Usalama wa wahudumu wa masuala ya kibinadamu ambayo ni ya mwaka 1997.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii