Makonda Arejea Afanya Ukaguzi wa Uwanja wa ndege Arusha

MKUU wa Mkoa wa ArushaPaul Christian Makonda leo Agosti 16, 2024 amefanya ukaguzi wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 2.7 zimetumika katika ujenzi wa mradi huo wa jengo la abiria pamoja na usimikaji wa miundombinu mbalimbali wa mifumo ya usalama na mfumo wa uzimaji moto, mfumo wa taarifa za ndege na abiria (AMIS).

Jengo hilo likikamilika litahudumia abiria 1,000 kwa siku na 600,000 kwa mwaka pia wanategemea kuweka taa ili uwanja utumike saa 24.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii