Nape" Sina Akauti yoyote ya mtandao wa kijamii inayofanya kazi kwa sasa"

MBUNGE wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ameutahadharisha Umma wa watanzania kwamba hana akauti yoyote ya mtandao wa kijamii inayofanya kazi kwa sasa (iliyo-active).


Nape amelazimika kutoa ufafanuzi huu kutokana na kuibuka kwa akaunti hasa katika mtandao wa X zinazoandika vitu mbalimbali zikiwa na jina la Nape Nnauye na kufanya kama ni yeye amezungumza au kutoa maoni yake, kitu ambacho amesema sio kweli na kusisitiza kuwa hausiki nazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii