Nchini DRC, chama cha rais, Union for Democracy and Social Progress (UDPS), kinazama zaidi katika mgogoro unaokikabili kwa sasa. siku ya Jumapili hii, Augustin Kabuya, kiongozi wa chama hicho cha rais kwa miaka miwili, ameachishwa kazi na bodi ya nidhamu iliyokutana, ambapo baadhi ya wapinzani wake wanaomtuhumu hasa kwa utovu wa nidhamu, kutokuwa na maono, upendeleo na mambo mengine ya kupinga maadili. Mvutano huo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa, lakini umefikia kilele chake.
Mwezi Februari 2022, CDP, chombo cha nidhamu cha UDPS kilimteua Augustin Kabuya, wakati huo akiwa naibu katibu mkuu wa chama, kuwa kiongozi wa chama. Zaidi ya miaka miwili baadaye, ni chombo kile kile ambacho kinamtimuwa, Mkataba ambamo tunampata naibu André Mbata. "Ilikuwa siku nzuri ambayo inaashiria mwanzo wa kuzaliwa upya kwa chama. Tumemfahamu mtu ambaye kiuhalisia alikuwa mmoja wa viongozi masikini wa chama hiki ilhali ni lazima tumuunge mkono kiongozi na tubaki na madaraka kwa muda mrefu iwezekanavyo", amesema mbunge wa chama cha UDPS André Mbata.
Déo Bizibu, naibu wa Kabuya, amepewa jukumu la kuongoza chama cha UDPS kwa muda. “Wiki ijayo tutakuwa na mkutano usio wa kawaida na tukipitia kila kitu kilichotokea, tutapata tiba. Hatufanyi hivyo peke yetu. Ni lazima iwe sambamba na mamlaka ya kumbukumbu ya chama, na watendaji wengine wa chama kupitia mashauriano yatakayofanyika. Pia kuna maswala mengi hatarini kuhusiana na mwaka 2028.
Ikiwa Augustin Kabuya hakutaka kujibu maombi yetu kwa kuweza kueleea kilichotokea, wasaidizi wake wanapinga uhalali wa mkutano ambao ulimfuta kazi. Kulingana nao, Augustin Kabuya anasalia kuwa kiongozi wa UDPS. "Rais Félix Tshisekedi pekee ndiye anayeweza kuamua vinginevyo," anasema mmoja wa marafiki zake wa karibu, ambaye kwa sasa yuko serikalini.
Rais Tshisekedi alielezea mvutano huu kama "uhai wa kidemokrasia", akitarajia kurejea kwa utaratibu bila kudhoofisha chama. Kwa sasa, makao makuu ya UDPS yanasalia kudhibitiwa na kambi ya Augustin Kabuya iliyodhamiria kuwapinga wale aliowataja hivi majuzi kuwa watenda wavuvi wanaovua katika maji hatari.