Mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez akataa wito wa Mahakama ya Juu

Wakati Nicolas Maduro, anayeshukiwa kwa udanganyifu katika uchaguzi wa urais, alikata rufaa katika Mahakama ya Juu zaidi ili uchaguzi wa Julai 28 uchunguwze, mahakimu wake walitoa hati ya kumwitisha mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez kufika mbele yao Agosti 7. Alikataa kufika mbele yao, kwa kuhofia kukamatwa.

"Nikienda katika Mahakama ya Juu zaidi, nitakuwa hatarini kabisa", Hivi ndivyo Edmundo Gonzalez amehalalisha kutoitikia kwake wito wa mahakama kuu ya Venezuela siku ya Jumatano, Agosti 7, ambayo kwa sasa ina jukumu la kuchunguza mchakato wa uchaguzi wa Julai 28. Hata hivyo katika barua iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii, mgombea huyo wa upinzani anaongeza " nitahatarisha sio tu uhuru wangu, lakini pia matakwa ya wananchi wa Venezuela". Wakati huo huo wawakilishi wa vyama vilivyounga mkono ugombea wa Edmundo Gonzalez kwa uchaguzi wa rais.


Tuliambia baraza la uchaguzi kuwa hatuelewi sababu ya kuwepo kwetu. Kwa sababu taasisi pekee iliyoidhinishwa kufanya mchakato wa uchaguzi, kujumlisha kura na kutangaza matokeo, ni Baraza la Taifa la Uchaguzi.”


Chumba cha uchaguzi cha Mahakama ya Juu kina siku kumi na tano ambazo zinaweza kuongezwa kuchunguza mchakato mzima wa uchaguzi, na haswa taarifa fupi za vituo vya kupigia kura ambazo bado hazijawekwa wazi na Baraza la Taifa la Uchaguzi, jambo ambalo linasukuma Wavenezuela na jumuiya ya kimataifa kuchukulia kuwa kulikuwepo na udanganyifu mkubwa katika kutangaza matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo kuna uwezekano mdogo kwamba Mahakama itafafanua swali hili;


Upinzani unadai, kwa upande wake, kuwa umeshinda uchaguzi wa urais, madai ambayo yanaoungwa mkono na nchi kadhaa zikiwemo Marekani na Argentina.


Kwa upande wake, jeshi linakataa mwito wa upinzani kuunga mkono, likiita wito huo wa "kukata tamaa na uchochezi". Na limerejelea "utiifu wake kabisa" kwa rais Maduro. Kwa hivyo kwa nini uungwaji mkono huu usiotetereka wa jeshi kwa Nicolas Maduro? Mtaalamu wa masuala ya siasa Andrei Serbin Pont, kiongozi wa CRIES, taasisi inayojishughulisha na masuala kuhusu Amerika ya Kusini na Karibiani, ameelezea haya kwa Hugo Passarelo wa timu ya wahariri ya lugha ya Kihispania.


"Tukumbuke kwamba jeshi la Venezuela sio tu ambalo linaweza kutekeleza vurugu kwa jina la serikali."


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii