Rais wa DRC Félix Tshisekedi hapo jana, amemshutumu mtangulizi wake, Joseph Kabila, kwa kuchochea mzozo wa usalama mashariki mwa DRC kupitia Muungano wa (AFC).
Katika mahojiano na Radio Top Congo, akiwa Brussels (Ubelgiji) ambako amekaa kwa siku chache kwa sababu za matibabu, Tshisekedi amesema alijaribu kuwasogelea wapinzani wake, lakini hawataki.
“Nilichukuwa mfano wa wapinzani watatu, nilianza na Martin Fayulu hajawahi kamwe kukubali matokeoa ya uchaguzi, atakubali vipi ukaribu na mimi.” Alisema Rais Félix Tshisekedi.
Aidha ameeleza kwamba Moise Katumbi naye alikuwa na msimamo huo huo lakini kutokana na shinikizo kutoka upande wake, alikubali kuingia kwenye taasisi lakini anabaki nje.
Kwa mujibu wa rais Tshisekedi, Joseph.Kabila naye aklikataa kushirki uchaguzi, na anapanga kuendesha vurugu, sababu AFC ni yeye.
Mbai na hilo Felix Thisekedi amesema kamwe hawezi kuketi kwenye meza moja ya mazungumzo na M23 na washirika wake AFC