Ukraine yaikosowa Mali kukata mahusiano

Ukraine imekosoa hatua ya Mali kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na Kyiv na kuuita kama “uamuzi usiiona mbali” na uliochukuliwa haraka bila ya kufanya uchunguzi wa kina.

Ukraine imeeleza kuwa hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuonyesha kuwa nchi hiyo imehusika kwa namna yoyote ile katika mapigano yaliyosababisha vifo vya wanajeshi wa Mali na mamluki wa kundi la Urusi la Wagner.

Wizara ya mambo ya nje ya Ukraine imetoa taarifa hiyo kwenye tovuti yake baada ya Mali kutangaza jana Jumapili kwamba inakata mara moja uhusiano wake na Kyiv baada ya msemaji wa shirika la ujasusi la kijeshi la Ukraine kukiri kwamba nchi hiyo ilihusika katika mapigano yaliyosababisha vifo vya wanajeshi wa Mali na wapiganaji mamluki wa Wagner.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii