Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Alhamisi usiku na kumhakikisha kuwa Marekani iko tayari kulinda usalama wa Israel dhidi ya vitisho vyote vya Iran.
Iran iliapa kukuifanyia kipigo kikubwa iSrael kufuatia kifo cha kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh. Siku ya Alhamisi Kiongozi wa Hezbollah kutoka Lebanon Hassan Nasrallah amesema kwamba Israel inapaswa kutarajia "jibu lisiloepukika" kutoka kwa kundi lake baada ya mauaji ya kiongozi wake wa kijeshi Fouad Chokr siku ya Jumanne karibu na mji wa Beirut .
Ikulu ya White House imeeleza hayo baada ya kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Hanniyeh mjini Tehran pamoja na kamanda wa kijeshi wa Hezbollah Fuad Shukr mjini Beirut.
Naye Makamu wa rais wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris, alijiunga pia na mazungumzo hayo na kwa pamoja wakasisitiza kuwa juhudi zinaendelea ili kupunguza hali ya mvutano mkubwa huko Mashariki ya Kati.
Hata hivyo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Israel Tel Aviv kufuatia vitisho kutoka makundi ya Hamas, Hezbollah na Wahouthi ambayo yanafadhiliwa na Iran.