Changamoto za ulimwengu zinaongezeka na Afya inazorota; Anasema Guterres

Mamilioni ya watu Sudan na Gaza wako hatarini kufa sio tu kutokana na risasi na mabomu lakini majeraha yasiyotibiwa na magonjwa

Baraza Kuu la 77 la Shirika Afya Duniani lilifungua kikao chake cha kila mwaka cha wiki nzima Jumatatu kwa maelezo ya kawaida, wakati wajumbe walikuwa wanakabiliwa na jukumu la kuweka sera za afya kwa mwaka ujao huku kukiwa na changamoto kubwa kwa ustawi wa ulimwengu kutokana na migogoro mingi ambayo, katika baadhi ya maeneo, ilitishia kufuta miongo kadhaa ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliambia baraza hilo kwa njia ya video kutoka New York nchini Marekani, kwamba dunia inakabiliwa na matatizo na kwamba afya ya ulimwengu inataabika “kuanzia machafuko ya hali ya hewa hadi kuongezeka kwa umaskini na ukosefu wa usawa, na kuzidisha migogoro”.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii