Palestine yakaribisha hatua ya Ireland, Norway na Uhispania kuitambua kama taifa

Mamlaka ya Palestine ambayo kimataifa inatambuliwa kama mwakilishi rasimi wa watu wa Palestine imekaribisha hatua ya nchi za Ireland, Norway na Uhispania kutambua eneo hilo kama taifa, ikisema ni kitendo cha kihistoria.

Kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa X, katibu mkuu wa mamlaka hiyo Hussein al-Sheikh amesifia hatua hiyo ya IrelandNorway na Uhispania.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii