China yawekea vikwazo makampuni ya Marekani yanayouza silaha kwa Taiwan

China imeweka vikwazo vipya dhidi ya makampuni matatu ya Kimarekani yanayouza silaha kwa Taiwan, ambapo Rais Lai Ching-te ameapishwa leo Jumatatu, Mei 20, 2024, limeripoti shirika rasmi la Habari la China.


Kampuni za General Atomic Aeronautical Systems, General Dynamics Land Systems na Boeing Defense, Space & Security zitawekwa kwenye orodha ya serikali ya China ya "vitu visivyotegemewa", vyombo vya habari vya serikali vimesema, vikinukuu Wizara ya Biashara.

"Watapigwa marufuku kutoka kwa shughuli yoyote ya kuagiza-nje iliyounganishwa na China na kupigwa marufuku kutoka kwa uwekezaji wowote mpya nchini China," kulingana na vyombo vya habari. "Watendaji wakuu wa makampuni haya wamepigwa marufuku kuingia China, na vibali vyao vya kazi vitafutwa," ameongeza.

Tangazo la rais mpya wa Taiwan anayeingia madarakani

Tangazo hilo linakuja wakati rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te akiingia madarakani Jumatatu, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa China. Anamrithi Tsai Ing-wen ambaye miaka minane madarakani iliambatana na kuzorota kwa uhusiano na Beijing.

Beijing inachukulia Taiwan kuwa moja ya majimbo yake kuunganishwa tena kwa nguvu ikiwa ni lazima na imemtaja Lai Ching-te kama "mwanaharakaiti wa hatari wnaotaka kujitenga" ambaye ataongoza Taiwan kwenye njia "ya vita na kushuka kwa uchumi." Ikiwa Washington imeitambua Beijing kwa hasara ya Taipei tangu 1979, Bunge la Marekani wakati huo huo limetangaza kupia  wa silaha Taiwan, kwa lengo lililowekwa la kuiondoa China kutoka kwa nia yoyote ya kujitanua.

Mnamo mwezi wa Aprili 2024, Marekani iliidhinisha dola bilioni kadhaa za msaada wa kijeshi kwa Taiwan. Msaada huu ni sehemu ya mpango mkubwa wa dola bilioni 8 wa kusimama mbele ya China kijeshi kwa kuwekeza kwenye nyambizi, na kiuchumi kwa kushindana na miradi mikubwa ya China katika nchi zinazoendelea.

Msaada wa kijeshi ambao huongeza "hatari ya migogoro", Beijing ilijibu mara moja. "Marekani lazima [...] ikome kuipatia Taiwan silaha, ikome kuunda mivutano mipya katika Mlango-Bahari wa Taiwan na kuacha kuathiri amani na utulivu katika pande zote za mlango huo," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii