Dkt. Ashatu Kijaji Ateuliwa Kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akichukua nafasi ya Dkt. Selemani Jafo ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.


Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.


Rais Samia amemteua pia Mhandisi Yahya Ismail Samamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini akichukua nafasi ya Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.


Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Samamba alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii