Wanawake waandamana Ufaransa

Maelfu ya wanawake waliingia barabarani katika miji ya Ufaransa, Jumapili kupinga maandamano ya kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen, huku kura za maoni zikionyesha kuwa chama hicho kinaweza kushinda uchaguzi ujao wa bunge.

Takriban makundi 200 ya haki za wanawake na vyama vya wafanyakazi yaliandaa maandamano hayo katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Paris, wakisema haki za wanawake zinakabiliwa na mashambulizi kutoka nchi zinaongozwa na vyama vya siasa kali.

Jijini Paris, zaidi ya wanawake 10,000 waliandamana kwa amani, waandaaji wamesema.

Mwezi Machi, Ufaransa iliweka haki ya kutoa mimba katika katiba yake, likiwa ni shauri la kwanza duniani, lakini baadhi ya wabunge wa RN walipinga sheria hiyo, na kuibua wasiwasi miongoni mwa baadhi ya watu katika umma kuhusu mitazamo ya chama hicho juu ya haki za wanawake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii