cha kwanza cha Bunge kitafunguliwa mjini Cape Town leo Ijumaa, Juni 14, karibu saa 4 asubuhi, tangu uchaguzi wa wabunge mwezi uliopita, ambao ulishuhudia ANC, chama kilichokuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, kupoteza wingi wake kamili. Kwa hivyo ANC italazimika kuunda miungano ili kuunda serikali ya mseto. Vyama kadhaa vya upinzani tayari vimeonyesha kuwa vitajiunga na serikali hii ya umoja wa kitaifa. Lakini serikali hii ya muungano haiwaridhishi watu wote.
Nchini Afrika Kusini, kuna hatari kikao hicho kikumbwe na mvutano. Leo Ijumaa, Wabunge watakula kiapo kabla ya kumchagua rais na naibu spika wa Bunge hilo. Kisha utakuja uchaguzi wa Rais wa Jamhuri, kwa wingi wa kura. Kwa miaka 30, kumchagua rais wake ilikuwa ni utaratibu wa ANC.
Lakini kwa mara ya kwanza, Rais Ramaphosa, mgombea anayetaka kuchaguliwa tena, atafika mbele ya Bunge bila wingi kamili, anaripoti mwandishi wetu huko Cape Town, Romain Chanson. Chama hicho, hata hivyo, kinasalia kuwa chama kikubwa zaidi cha kisiasa katika baraza hilo lenye wabunge 159 kati ya 400.
Hata hivyo siku ya Alhamisi chama cha ANC kilitangaza kuwa kimekamilisha makubaliano ya serikali na vyama kadhaa kwa nia ya kuunda serikali ya mseto.
Tumefikia makubaliano ya pamoja juu ya haja ya kufanya kazi pamoja," katibu mkuu wa ANC Fikile Mbalula amesema katika mkutano na waandishi wa habari. Muungano lazima "uelekee katikati" na ujumuishe chama cha mrengo wa kati cha Democratic Alliance (DA), chama cha Kizulu cha Inkatha Freedom Party (IFP), pamoja na vyama vingine vingi vidogo, alisema.
IFP, chama kidogo cha Wazulu, kinajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa iliyopendekezwa na ANC
ANC, chama tawala, kilishindwa kupata wingi wa kura katika chaguzi zilizopita na kimeanzisha majadiliano na vyama kadhaa vya upinzani kwa nia ya muungano. Siku ya Jumatano, Juni 12, IFP, chama kidogo cha Wazulu, kilitangaza kuwa kinajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa, iliyopendekezwa na ANC. "Ni wakati wa Inkatha Freedom Party kuimarisha serikali," kiongozi wake Velenkosini Hlabisa alitangaza siku ya Jumatano, Juni 12, wakati wa mkutano na wanahabari. "Tunatanguliza uthabiti na maslahi ya Afrika Kusini," aliongeza, "kama tulivyoahidi kufanya katika muda wote wa kampeni za uchaguzi. " Chama hicho kilishika nafasi ya tano kwenye uchaguzi na kitakuwa na wabunge 17 katika bunge jipya.