Katika mtandao wa kijamii wa X, Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani inayounga mkono operesheni ya kupeleka msaada wa ziada wa kibinadamu kwa raia wa Palestina wanaohitaji, imesema malori ya kupeleka msaada yataanza kusonga mbele kwenye pwani hiyo leo. Ujenzi wa bandari hiyo ya muda ulitangazwa mwezi Machi na Rais Joe Biden na kujengwa kwa gharama ya takriban dola milioni 320, ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kukwepa vizuizi vya ardhini kuingia katika Ukanda wa Gaza vilivyowekwa na Israel, mshirika wa karibu wa Washington.Wakaazi wa Rafah wako hatarini kushambuliwa na Israel Haya yanajiri huku Israel ikidai kuwa wanajeshi wake watano wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa ufyatulianaji risasi katika vita vya Gaza. Kwa mujibu wa jeshi watano hao waliuawa wakati vifaru viwili vya Israel vilirusha makombora kwa makosa katika jengo walimokuwa wakati wa mapigano katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumatano.