Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema zaidi ya wanachama 1,000 wa kundi la Hamas wanapokea matibabu nchini Uturuki.
Rais Erdogan ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.
Kiongozi huyo wa Uturuki hata hivyo hakutoa maelezo zaidi juu ya sehemu walikojeruhiwa wanachama hao wa Hamas au jinsi walivyofika Uturuki.
Erdogan amewahi kuieleza Hamas kama kundi la ukombozi linalotetea haki za Wapalestina.
Hata hivo, Marekani, Uingereza, Israel na mataifa mengine yenye nguvu yameliorodesha Hamas kama kundi la kigaidi.