Holcim Group yaiweka sokoni Mbeya Cement

Kampuni kubwa ya Saruji ya Uswizi imetangaza mpango wa kuuza kampuni yake tanzu Pan African Cement, ambayo inashikilia asilimia 65 ya Kampuni ya Saruji Mbeya (Mbeya Cement), kwa Kampuni ya Amsons Group.

Hatua ya kujiondoa katika soko la Tanzania, kulingana na taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki, inalenga kuoanisha mkakati wa Holcim wa 2025, ‘Kuharakisha Ukuaji wa Kijani’ ambao unalenga katika kuimarisha uongozi wake katika masoko ya msingi.

“Kampuni ya Holcim Group imefikia makubaliano na kampuni ya Amsons Industries (T) Ltd ya kuiuzia kampuni yake tanzu ya Pan African Cement Limited, ambayo ina hisa asilimia 65 katika kampuni ya Mbeya Cement,” amesema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Holcim’s Lafarge Tanzania, Medhat Ismail katika taarifa aliyoitoa jana.

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo Ismail aliiongeza katika taarifa yake hiyo kuwa mchakato wa kuuza kampuni hiyo tanzu ya Pan African Cement kwenda Kampuni ya Amsons Group, uko katika hatua ya kuidhinishwa na mamlaka husika za serikali.

“Tumefurahi kupata mshirika wa kimkakati na anayeaminika wa biashara huko Amsons Group, ambayo iko katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwekeza katika ukuaji wake wa muda mrefu,” aliongeza Ofisa Mtendaji huyo.

Kiwanda hicho cha Mbeya Cement kinadhamani ya dolla za Kimarekani milioni 170, taarifa hiyo ilisema, shughuli za kampuni ya Mbeya Cement zitaendelea bila usumbufu, na kudumisha kasi na viwango vya biashara.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii