Katibu Mkuu CWT asimamishwa

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama wa Walimu Tanzania CWT imemsimamisha kiutendaji Katibu Mkuu wa chama hicho Josephat Maganga, kwa tuhuma za uvunjifu wa katiba ya Chama na kanuni zake ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na fedha.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania Thobias Sanga, ambae ni mwakilishi wa Walimu kutoka Njombe, amesema kuna changamoto kubwa katika utendaji hasa matumizi ya 2% makato ya mshahara wa walimu.

Kikao hicho kimefanyika chini ya mti kikiwa na wajumbe 18 kati ya 32 wa Kamati ya Utendaji ya Taifa ya CWT, wakimsimamisha kiutendaji katibu mkuu wa chama hicho hadi pale tuhuma zake zitakapofikishwa Katika baraza kuu.Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii