Ali Kamwe, Mobeto wadaiwa wapenzi

Inadaiwa kuwa Afisa Habari wa Klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe na Mrembo Hamisa Mobeto wapo kwenye penzi la moto, hii imekuja baada ya wawili hao kupostiana kwa nyakati tofauti kwenye kurasa zao za Instagram (Instastory).

Kwa upande wa Kamwe alishare picha ya Hamisa na kuisindikiza na neno RAHA, huku Hamisa naye alishare picha ya Ali Kamwe na kuisindikiza na Kopa La Moto.

Kwa upande wa Digital Manager wa Klabu ya Yanga SC, Privaldinho alishare ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akijiita Shemeji Yake Hamisa kitu ambacho wengi wameconnect kuwa Hamisa na Kamwe ni wapenzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii