Msanii wa Hip Hop Young Jeezy wa Marekani amekataa kutumia neno "OG" kulinganana na maana ya neno hilo.
Neno OG maana yake ni ORGINAL GANGESTER na neno hili hata bongo huwa linatumika kulingana na mtumiaji mwenye na dhana yake.
Lakini kwa upande wa marekani mtu ambaye ni ORGINAL GANGESTER mara nyingi huwezi kujifunza chochote kutoka kwa mtu huyo, wakati kwenye maisha watu wengi hujifunza kutoka kwa watu wengine na kufanikiwa kutokana na kile alichijifunza.
Pia ni mtu amabye hawezi kupenda kile ambacho mwingine anakifanya, halikhalika hata ukikosea OG hawezi kusema wala hawezi kukurekebisha.
Young Jeezy yeye anapenda neno BIG HOMIE na sababu zinazopelekea yeye kutumia neno hilo ni kwamba BIG HOMIE ni mtu ambaye huwa anapenda kitu kingine ambacho mtu anafanya, kujifunza kutoka kwa mingine na huwa ni mtu ambaye huwa ana unga mkono vitu vya watu wengine.