Serikali za Burkina Faso na Niger zimetoa taarifa ya pamoja inayosema kwamba majeshi yake yameua wapiganaji wa kiislamu 100 katika oparesheni ya wiki mbili.
Hakuna ripoti huru kudhibitisha madai hayo ambayo yametolewa baada ya rais wa Burkina Faso Roch Kabore kumfuta kazi waziri mkuu kufuatia maandamano ya raia kulalamikia ongezeko la mashambulizi ya wapiganaji.
Raia 13 wanaopigana na makundi ya wanajihadi waliuawa jana alhamisi kaskazini mwa nchi hiyo.
Kundi la wapiganaji wa kujitolewa liliundwa miaka mitatu iliyopita katika juhudi za kumaliza nguvu kundi la wapiganaji wa kiislamu.
Zaidi ya wanachama wake 250 wameuawa.
Wanajeshi na polisi kadhaa vile vile wameuawa katika mda wa mwaka mmoja.