Jeshi la Polisi Tanzania limeteketeza silaha 5,230 haramu zilizokamatwa katika kipindi cha miaka miaka minne kuanzia mwaka 2018 hadi Oktoba 2021.
Zoezi hilo limefanyika leo Ijumaa Desemba 10, 2021 katika Viwanja vya Shabaha vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) vilivyoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Christopher Kadio amesema suala la ulinzi na usalama ni la maendeleo ya mtu mmoja mmoja kama hakutakuwa na amani, maendeleo hayawezi kupatikana.
Amesema silaha haramu zinaweza kuathiri uchumi wa nchini kwa kuwa wahalifu wamekuwa wakitekeleza vitendo vya kijangili.
"Silaha hizi zingebaki mkono mwa wananchi zingeleta madhara makubwa hasa kwa wafanyabiashara na kusababisha ucheleweshaji wa ukuaji wa uchumi,"amesema Kadio.
" Miongoni mwa silaha haramu zinazoteketezwa silaha 2, 628 zilipokelewa kutoka polisi wa wanyama pori ambapo zilikuwa zilitumika kwenye vitendo vya kigaidi, "amesema.