FARU WA TANZANIA SASA RUKSA KUOA KENYA.

Wakati Tanzania ikiipatia Kenya ndege aina ya Korongo 20 kama zawadi ya Kristimas, Kenya imekubali Faru wa Tanzania waoe Kenya.

Ndege 20 waliotolewa kwa Kenya kutaifanya nchi hiyo kuwa na ndege hao 32 kutoka 12 waliopo sasa kwani Tanzania ilikuwa nao 4000.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Desemba 10, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifafanua baadhi ya maeneo ambayo yamewekewa makubaliano kati ya nchi hizo mbili ikiwemo utalii, nishati, ulinzi wa mipaka na sekta ya afya.

Katika sekta ya utalii, Mhe. Samia amesema ikolojia ya Tanzania na Kenya ni moja ila imegawanywa na mipaka huku akibainisha kuwa wamewataka mawaziri wa eneo hilo kukaa, kuzungumza na kuondosha changamoto ili nchi zifaidike kuleta watalii wengi na kupata mapato.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii