Marekani yamuwekea vikwazo Jenerali wa jeshi la Uganda

Wizara ya fedha ya Marekani imemuwekea vikwazo mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi la Uganda, Meja Jenerali Abdel Kandiho, kwa shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu zilizofanyika chini ya uangalizi wake.

Jeshi la Uganda limesikitishwa na uamuzi huo na litahitaji ufafanuzi kutoka Washington, ikizingatiwa Kampala ni mshirika wa kiusalama dhidi ya wanamgambo wa eneo la Afrika Mashariki katika miaka ya hivi karibuni.

Wizara ya fedha imetangaza mfululizo wa vikwazo wiki hii kuadhimisha mkutano demokrasia wa rais wa Marekani, Joe Biden, ukilenga watu inaowaona wanajihusisha na rushwa, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ambao wanadumaza demokrasia.

Chini ya Meja Jenerali Kandiho, wizara ya fedha imesema katika taarifa yake, maafisa wa ujasusi katika jeshi, iliwashikilia na kuwanyanyasa Waganda walio ikosoa serekali ya Uganda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii