MGOMBEA URAIS NCHINI KENYA AMEAHIDI MIKOPO KWA WATAKAOOANA.


Mtia nia wa kugombea urais nchini Kenya ameahidi kutoa mikopo yenye thamani ya kati ya TZS milioni 10 hadi TZS milioni 20 kwa wanandoa wapya endapo atachaguliwa katika ofisi hiyo ya juu zaidi nchini humo.


Aidha, amesema kuwa serikali yake itaelekeza kwamba upandaji miti uchukuliwe kama sehemu ya mahari. "Unapokwenda kulipa mahari, utatakiwa kusema na idadi ya miti uliyopanda."

Gavana wa Machako, Alfred Mutua amesema hayo wakati akizindua ilani yake ya uchaguzi na kusema mikopo hiyo ya riba nafuu italipwa ndani ya miaka 20, na kwamba itawezesha wanandoa wapya kuanza maisha kwa wepesi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii