Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa Variety, rappa Drake amejiondoa kuwania tuzo za Grammy 2022.
Mmoja wa wawakilishi wa tuzo hizo amefunguka kuwa uongozi wa Drake umefikia hatua hiyo na hakuna maelezo yoyote ya kina yaliyotolewa.
Tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kutolewa Januari 31, 2022, Drake anawania kwenye vipengele viwili ambavyo ni Best Rap Album (Certified Lover Boy) na Best Rap Performance kupitia wimbo wake (Way 2 Sexy) ambao amewashirikisha Future na Young Thug.