WEMA SEPETU " SIWEZI KUCHORA TATOO YA MWANAUME BABA YANGU YUPO".

Wema Isaac Abraham Sepetu siku hizi wanamuita Last Born wa Taifa; ni staa mwenye jina kubwa kunako Bongo Movies ambaye anafunguka kuwa, kamwe hawezi kuchora tattoo ya jina la mwanaume kwenye mwili wake kwa sababu hakuna mwanaume wa kumuamini zaidi ya mzazi wake ambapo yeye amemchora baba yake mzazi, marehemu Balozi Sepetu.

 Wema au Tanzania Sweetheart anasema kuwa, hakuna kitu ambacho mwanaume anaweza kumfanyia chenye maajabu makubwa kwake kiasi cha kumchora tattoo hivyo kamwe hawezi kuchora jina la mwanaume yeyote kwenye mwili wake zaidi ya wazazi wake  au watoto wake akibarikiwa na si vinginevyo.

“Yaani mwanaume ambaye nimempa nafasi ya kumchora mwilini wangu ni baba yangu peke yake na si mtu mwingine yeyote maana sijaona maajabu aliyofanya mwanaume kwangu mpaka niende kabisa  kumchora na hata akiyafanya bado hana nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu kabisa maana hata kwa Mungu nitaulizwa juu ya hilo,” anasema Wema.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii