SERIKALI KUAINISHA CHANGAMOTO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Amesema Serikali Itaendelea Na Utaratibu Wa Kuzianisha Changamoto Zote Zinazorudisha Nyuma Sekta Ya Uwekezaji Na Kuzitafutia Ufumbuzi Ili Kuendelea Kuvutia Wawekezaji Wengi Kuwekeza Hapa Nchini .


Rais Samia Ameyasema Hayo Wilaya Ya Kigamboni Dar Es Salaam Wakati Wa Uzinduzi Wa Kiwanda Cha Kutengeneza Vifaa Vya Umeme Cha Elsewedy Electric Africa Limited Na Kuongeza Kuwa Serikali Iteendelea Kuweka Miundombinu Wezeshi Ikiwamo Sheria Na Sera Za Biashara Ili Kuleta Tija Katika Sekta Ya Uwekezaji.

Pia Rais Samia Katika Uzinduzi Huo Ameweka Bayana Safari Ya Uwekezaji Hapa Nchini Kuwa Bado Inaendelea Katika Maeneo Mbalimbali .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii