Tani laki tatu za sukari kuingizwa nchini

Serikali imesema kuwa zaidi ya tani laki tatu za sukari zinatarajiwa kuingizwa nchini mwaka huu kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa sukari.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya Habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi ya Norway, Vatican na Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri Bashe amesema kuwa haki kufikia Machi mwaka huu tani 60,000 za sukari zitakuwa zimefika nchini hivyo wanatarajia hasi kufikia mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani hali itakuwa shwari.

“Tutaendelea kuingiza sukari nchini na tumeitumia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), hii sukari inayoingia sasa hivi imeletwa na kampuni iliyoingia makubaliano na NFRA na siyo viwanda kwa sababu hili ni suala la usalama wa nchi na chakula.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii