Elon Musk kushitakiwa Brazil

Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil, Alexandre de Moraes, ameanzisha uchunguzi dhidi ya mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, Elon Musk.


Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Musk anatuhumiwa kwa kuzuwia sheria kuchukuwa mkondo wake.

Mmiliki huyo wa mtandao wa X anapingana na uamuzi wa Jaji Moraes ulioutaka mtandao huo wa kijamii kuzifungia baadhi ya akaunti za watumiaji.

Mapema hapo jana, Musk alituma ujumbe kwenye mtandao huo akisema X itaondowa zuio dhidi ya watumiaji hao kwa kuwa ni kinyume na katiba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii