Vita kati ya Israel na Hamas vyaingia mwezi wa sita

Vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas vimeingia mwezi wake wa 6, huku Marekani na wapatanishi wengine wakitarajiwa kujiunga na wenzao wengine mjini Cairo kujaribu kufikia makubaliano juu ya usitishwaji wa mapigano.



Ujumbe wa Cairo pia utajadili hatua za kuachiwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika ukanda wa Gaza.

Kulingana na shirika la habari la Misri Al-Qahera, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi, CIA, Bill Burns na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, watajiunga na ujumbe wa wapatanishi mjini Cairo na kuwa na mazungumzo ambayo sio ya moja kwa moja na maafisa wa Qatar na Hamas. 

Hamas ilithibitisha kwamba moja ya matakwa yake katika mazungumzo hayo ni kusitishwa kabisa mapigano mjini Gaza na wanajeshi wa Israel kuondoka huko. 
 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii