Israeli yaendelea kutekeleza mashambulio mazito dhidi ya Hamas

 Wanajeshi wa Israeli wameendelea kutekeleza mashambulio mazito dhidi ya wapiganaji wa Hamas, pembezoni mwa hospitali kadhaa kwenye ukanda wa Gaza, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa kwa vita.


Haya yanajiri wakati huu mchakato wa mazungumzo unaoongozwa na Marekani na Misri, kusaidia kupata suluhu ukionekana kutozaa matunda nchini Qatar.

Wajumbe wa Israeli na Hamas, wanaoshiriki kwenye mazungumzo hayo wanalaumiana kuhusu kutopatikana kwa mwafaka.

Katika hatua nyingine, Marekani inapinga mpango wa Israeli wa kutuma wanajeshi wake wa ardhini kwenye mji wa Rafah wenye wakaazi Milioni 1.5.

Hata hivyo, Israeli inasema itaendelea na mpango wake, wanaosema utasaidia kuwaondoa wapiganaji wa Hamas, wanaojificha kwenye mji huo, ambao pia umeendelea kushambuliwa.

Wakati hayo yakijiri, kundi la Hezbollah ambao ni washirika wa Hamas, wamerusha maroketi kadhaa Kaskazini mwa Israeli na kusabisha kifo cha mtu mmoja, hatua inayokuja baada ya jeshi la Israli kuwashambulia Kusini mwa Lebanon.

Tangu kuanza kwa vita kati ya Jeshi la Israeli na Hamas tangu Oktoba 7 mwaka uliopita, Wapalestina zaidi ya Elfu 32 wemeuawa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii