Wanajeshi 150,000 wa Urusi wameuawa katika vita vya Ukraine

Ufaransa inakadiria kuwa wanajeshi 150,000 wa Urusi wameuawa tangu taifa hilo lilipoivamia Ukraine.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stephane Sejourne, amesema hayo kwenye mahojiano na gazeti la Urusi la Novaya Gazeta Europe yaliyochapishwa hii leo na kuongeza kuwa Paris inakadiria majeruhi kufikia 500,000.

Hata hivyo, Urusi haijachapisha taarifa zozote za uharibifu uliotokea katika vita hivyo vilivyoingia mwaka wa tatu.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alisema mwezi Februari kwamba wanajeshi 180,000 wa Urusi waliuawa, huku Uingereza ikisema karibu wanajeshi 450,000 wameuawa kwenye vita hivyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii