CAF yakataa ombi la Simba SC

Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmedy Ally amesema mchezo wao Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi Jwaneng Galaxy utachezwa Jumamosi Machi 2, 2024 saa 1:00 usiku, Licha ya Kupendeza kucheza mechi saa 10:00 jioni lakini CAF wameamua iwe saa 1:00 usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari Ahmedy Ally amesema kuwa Kikosi chao kimerejea nchini leo rasmi tunaanza mazoezi kujiandaa na mchezo Jwaneng Galaxy na mchezo wa ASFC dhidi TRA ambao tutacheza Jumatano kwenye uwanja wa Azam Complex.

“Ushindi wa aina yoyote ambao tutapata Jumamosi sisi tutafuzu bila kujali Wydad kapata ushindi wa aina gani. Sisi na Wydad tukishinda tutakuwa na alama tisa na kanuni ya kwanza ya CAF inaangalia Head to Head, mechi ya kwanza walitufunga goli 1-0 na sisi tukawafunga 2-0’’amesema Ahmedy.

Wakati huo huo Ahmedy amesema Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC.

‘’Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi”- Ahmed Ally.

Mechi ya kwanza kwa Simba kukutana na Jwaneg Ligi ya Mabingwa Afrika ilipokea kichapo cha mabao 3-1 Octoba 10, 2021 kwenye uwanja wa nyumbani na Octoba 27 mwaka huo ikashinda mabao 2-0 ikiwa ugenini.

Simba itaingia katika mchezo huu ikihitaji kulipa kisasi dhidi ya Jwaneng baada ya msimu wa 2021/22 kutupwa nje ya mashindano hayo kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini kufuatia mechi mbili baina yao kuisha kwa sare ya mabao 3-3.

Simba na Jwaneng Galaxy zimekutana mara tatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kila timu ikiibuka na ushindi mara moja na zimetoka sare moja.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii